27 August 2024
Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sasa iko ndani ya hatua ya utengenezaji wa michakato na mifumo ya sheria ya mpito, sauti ya wahanga na jamii zilizoguswa inapaswa kuchukua nafasi kubwa. Hakika, hakuna faida yoyote inayohusishwa na sheria ya mpito inayoweza kupatikana kwa gharama ya wahanga, bila ushiriki wao mkubwa. Maandishi hii inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti ambayo iliendeshwa mwaka wa 2023 kati ya watu 771 katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri. Washiriki walionyesha matarajio na uoga wao kuhusu amani na usalama kurejeshwa, utafiti wa ukweli, mashtaka, hatua za kuchukuliwa, hakikisho ya kutorudilia, na ukumbusho. Ujumbe hii inapendekeza hatua kwa watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa kuchukua katika utayarishaji na utekelezaji wa siasa inchini inayo husu sheria ya mpito katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.